Kutokana na masaibu ya zama zetu, ambapo tunakabiliwa na dhuluma, ukosefu wa huruma, upendo na imani, mwanadamu wa sasa amesongwa na kukabwa na ujinga wa zama za sasa. Njia pekee ya kuelekea kwenye tiba inapatikana katika kunufaika na siri kuu zinazopatikana ndani ya Nuru ya milele ya Muhammad (s.a.w).