Kuvuta pumzi ya mwisho ni jambo lisilokwepeka kwetu wanadamu. Swali muhimu kulitengezea majibu kwa wakati huu ni jinsi gani utaivuta? Kwa kila pumzi maisha yetu yanarefuka, lakini siku moja suala hili litasimama. Ustadh Othman Nuri Topbas ametupatia ukumbusho adhimu wa namna ya kujindaa na umauti ndani ya kitabu hiki, wapo walioishi maisha furaha yakeli lakini wakaikosa ladha nzuri ya pumzi hiyo wakatamani kuongezewa japo sekunde chache ili warekebishe hali zao hizo za mwisho na pia wapo walioishi pasi na kujali wala kufahamu umuhimu wa maandalizi ya jambo hili lakini mwisho wa uhai wao wakabadilika, wakaamini na kujikuta wakiivuta pumzi hiyo kati hali ya salama na amani.